PICHA :#RwandaDay : Utamaduni wa Rwanda ni gundi inayounganisha wanyarwanda. - Kagame

Rais Paul Kagame ameyasema haya maneno wakati alipokuwa hutubia tukio la Rwanda Cultural lililojumuisha wanyarwanda mjini San Francisco, Marekani kutoka Rwanda na kila kona za ulimwengu kwa kusherehekea utamaduni wa Rwanda na umuhimu wake baada ya mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya kitutsi.

Katika tukio hili, washiriki walijikumbusha maadili ambayo yanaunganisha kama wanyarwanda, jinsi walivyojitafutia ufumbuzi wa changamoto zilizowakabili baada ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi, kujijengea haki na maridhiano, kupunguza umaskini na kujijengea utawala bora.

Kagame aliwaambia washiriki kwamba kujenga upya Rwanda kuna msingi kwenye utamaduni ambako wananchi waliweka mbele maadili ya kupigania utu wao.

‘’utamaduni hana mmiliki, ni nyuzi inayounganisha na huleta kila mtu katika jamii. Tukiweka mbele manufaa ya wananchi, utamaduni unabadilika gundi inayowaunganisha watu wetu na utajiri usiokosa uzani.’’ Kagame alisema.

Kagame alitoa wito Waafrika kujitahidi kwa kujijengea Afrika ya kisasa na kuepuka kujifanya wazungu.

‘’Tunataka Afrika isio ingiliwa na wazungu. Mimi ni mwafrika anayeweza kujieleza kama mwafrika, mimi si ndio mwafrika aliyepotelea msituni akitafuta watu wenye rehema kumuonesha mwelekeo. Sijui kama mnasikia nini ninachofanya, lakini mnapaswa kusikiliza. Hakuna madaraka ambapo watu hawawezi kusikiliza wengine na ambapo sisi tunatarajiwa kumeza bila kutafuna vyovyote tunavyoambiwa . katika utamaduni wetu , tunatafuna kabla ya kumeza.’’ Kagame alisema.

Katika tukio hilo, utamaduni wa kila aina ulioneshwa na ukiwemo dansi za miondoko ya Kinyarwanda.


Watu mbalimbali walipongeza utamaduni wa Kinyarwanda, Mchungaji mashuhuri Mmarekani, Rick Wallen wa Saddliback church alisema kwamba yeye anaipenda Rwanda kwa mambo maalum mengi yaani ujasiri wa wanyarwanda, kusameheana , ukamilifu wa uongozi wa Rwanda, na kuwa Rwanda ni nchi iliyokataa kuingiliwa na viongozi wa kigeni.

Mmarekani mwingine, Michael Fairbanks ambaye ni mwanzilishi wa OTF Group na SABA Fund ambayo hutoa mafunzo ya kujiajiri na kutokomeza umaskini alisema kwamba yeye ameshatambua siri inayijificha nyuma ya mafanikio ya Rwanda.

‘’Kujitatulia matatizo kwa pamoja ni siri ya hadithi ya Rwanda, wanyarwanda ni watu wanaopenda ushindani na imani kwa kila mmoja.’’ Alisema.

Louise Mushikiwabo, waziri wa mambo ya kigeni na ushirikiano, pia msemaji wa serikali ya Rwanda, alisema kwamba duru za kuwa na ujumbe mmoja wa kushindana nchini kote ni juhudi zinazoendelea bila kusita.

Tukio liliwavutia watu zaidi ya 2,000 kutoka Rwanda na sehemu mbalimbali za Ulaya, Afrika, Asia , kama vile kutoka kila kona za Marekani na Kanada.

PICHA : tHE NEWTIMES

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments