Bomu laua mtu mmoja na watatu wamejeruhiwa, Nyanza

Watu wapatao watano (watoto wanne, kati ya 4 na 12 na mtu mzima mmoja,42) walilipua na Bomu la aina Gruneti kijijini Butare, tarafani Kigoma, wilayani Nyanza, kusini mwa Rwanda na mtu mmoja alifariki moja kwa moja na wanne wameripotiwa kujeruhiwa.

Habari kutoka mkoani kusini , zinasema kwamba hawa watu walikuwa wakisaka vyuma vilivyotupwa katika takataka na wakaliokota na wakaanza kuliponda kisha likalipuka.

Msemaji wa jeshi la polisi katika jimbo la kusini, CIP Andre Hakizimana alithibitisha hii ajali. ‘’ lilikuwa gruneti lenye umri, watoto walilichukua na wakaanza kuliponda mpaka likalipuka lakini wao hawakujua ni bomu au la.’’

Mpaka sasa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 12 ameshaaga dunia na wengine wawili, mmoja wa miaka 14 na wa 42 waliojeruhiwa vibaya wanatibiwa hospitalini ya Nyanza.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments