#Rwanda Day : Kagame ametakiwa kuwania urais mwaka 2017

Katika tukio la kitamaduni ‘Rwanda Cultural Day’ lililoanza mjini San Fransisco, Marekani ; wakati alipokuwa kupokea na kujibu maswali , mtu alisikika ndani ya ukumbi akimwomba Kagame kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi urais unaotarajiwa kufanyika mawka ujao.

Lorys Mundere, mnyarwanda anayeishi nchini Ubelgiji alijitokeza na akamuomba Kagame kuwa mgombea urais mwaka ujao.

‘’mnakumbuka kwamba katika historia walikuwepo Roosevert, DeGaule na Churchill, wakati wa hali ngumu, wanaume wenye uwezo wanatumia nguvu kwa kuokoa nchi zao, hii ndio sababu Bw Rais nataka wewe uwe mgombea urais mwaka wa 2017.’’

Mundere alisisitiza kwamba wanyarwanda wenyewe wanapaswa kuvisha Rais Paul Kagamwe medali ya mapongezi pasipo kutegemea medali ya kimataifa.

Lakini Kagame alimjibu kwamba medali halisi ni vitendo vya kujiendeleza.

Mwaka uliopita Wanyarwanda walichagua kurekebisha katiba ili kumruhusu Rais Paul Kagame kuingia kuwania muhula mwingine urais mwaka wa 2017, na yeye mwenyewe alisema kwamba hawezi kukataa maombi ya wanyarwanda ingawa yeye na chama chake RPF-Inkotanyi bado hawajathibitisha lolote kuhusu hivyo.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments