Rais Kagame na Gnassingbé wakutana mjini New York

Rais Paul Kagame na mwenzake Faure Gnassingbé, Rais wa Jamhuri ya Togo, walikutana jana mjini New York baada ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Septemba, 23, 2016.

Wao walijadili jinsi ya kuimarisha urafiki baada ya nchi hii ya Afrika Magharibi kushangazwa na jinsi ambavyo Rwanda iliweza kujijenga kiuchumi baada ya mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya Kitutsi katika mwaka 1994.

Gazeti la Republic of Togo limeandika kwamba wakuu wa nchi mbili walizungumzia biashara, maswala ya usalama katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na maswala mengi yanayojitokeza katika kanda ya maziwa makuu.

Rwanda inaendelea kufufua urafiki na mataifa ya magharibi mwa Afrika baada ya kuwatembelea marais wa Benin na Guinee Conakry ambapo walikubaliana kushirikiana kiuchumi.

Sasa, Paul Kagame yuko Nchini Marekani katika ziara ya kazi ambapo alipokutana na Benjamin Netanyahu katika mkutano kuhusu Teknolojia.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments