CAR : RDF wa kulinda amani wavishwa medali za mapongezi

Kikosi cha majeshi ya Rwanda wanaolinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wamevishwa medali za mapongezi na Uongozi wa MINUSCA.

Katika tukio lililofanyika Septemba,23, 2016, Haya majeshi ya Rwbatt3 wamepongeza kwa kufanya kazi kitalaam, ahadi na nidhamu .

Hili tukio la kuwavisha lilianzwa na gwaride la kijeshi katika kambi ya itwayo SOCATEL MPOKO iliyopo mjini Bangui.

Sherehe hii iliongozwa na naibu mkuu wa wajumbe wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Balozi Diane Corner aliyewashukuru sana askari wa Rwanda.

‘’tunawashukuru sana kwa kazi mliyofanya hapa, mlionesha ahadi, utaaluma na nidhamu kwa kutekeleza majukumu mliokubali.’’ Corner alitoa hotuba ya mapongezi kwa wanyarwanda.

Katika hotuba yake Luteni Kanali Claver Kirena aliyewakilisha majeshi ya Rwanda, alipongeza uongozi wa MINUSCA kuhusu ushirikiano wa dhati.

Kirenga alimbia washiriki kwamba walinda amani wa Rwanda katika kipindi cha miezi sita nchini CAR wanamlinda Rais, kuwalinda wananchi na kuisaidia serikali kujijenga

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments