Rwanda Cultural Day kutimua vumbi mjini San Francisco

Maelfu ya Wanyarwanda na marafiki zao wanaoishi nchini Rwanda na nchini za ugenini wanakutana kesho mjini San Francisco/California nchini Marekani kwa kusherehekea ‘Rwanda Cultural Day’’.

Hili ni tukio ambalo liliandaliwa na jamii ya wanyarwanda katika California kwa ushirikiano na Serikali ya Rwanda ili kusherehekea utamaduni wa Kinyarwanda na kujadili mabadiliko kiuchumi ya taifa.

Mkuu wa jamii ya wanyarwanda wanaoishi California, Yehoyada Mbangukira aliambia gazeti la The newtimes kwamba watu zaidi ya 2,500, wakiwemo watu wanaotoka Ulaya, Asia, Africa, na kutoka kila kona za Maerekani, wanatarajiwa kuhudhuria hili tukio.

Rais Paul Kagame atahutubia tukio katika majira ya alasiri mjini San Fransico ambapo tunapowazidi saa tisa.

‘’tunafurahi sana, ingawa hii si mara ya kwanza mimi kumuona Rais Kagame akiongea nasi katika matukio kama hili, tunajivunia kumleta hapa kwetu.’’
Mbangukira alisema.

Watu walioshiriki Rwanda Cultural Day za miaka jana wanasema kwamba wanavutiwa na hotuba za Kagame zenye ushauri, uzalendo, …

Tukio la mwaka jana lilifanyika mjini Amsterdm, nchini Uholanzi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments