Kagame aomba mataifa kuwaonesha wakimbizi rehema.

Rais Paul Kagame alisema kwamba walijadili mengi kuhusu namna ya kutafutia suluhu tatizo la wakimbizi lakini hakuna kitu kilichofanywa, Kagame alisisitiza kuwa hilo linapaswa kuwa kipaumbele.

Kagame aliyasema wakati alipokuwa kuhutubia mkutano mkuu wa umoja wa mataifa ambapo aliomba mataifa kuunga mkono zaidi shughuli za kulinda amani na usalama.

‘’ suala la wakimbizi na waomba hifadhi linapaswa kushughuliikiwa pasipo kungoja mpaka na mataifa yenye nguvu kuathirika.’’ Kagame alisema.

Vita nchini Syria na maisha magumu hasi katika nchi za Afrika ya kasikazini kulisababisha mlipuko wa wakimbizi na ongezeko la idadi ya watu wanaokwenda kujitafutia kibarua nchini za Ulaya.

Katika hotuba yake, Kagame alihusisha mipango ya SDGS na aliomba mataifa kujua kwamba maendeleo ya nchi moja ana uhusiano na ya nchi nyingine.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments