Mkutano wa kimataifa kuhusu Syria washindwa kupata ufumbuzi

Serguei Lavrov, John Kerry na Staffan de Mistura wakishiriki katika mkutano wa kimataifa kuhusu Syria mjini New York,

Mkutano wa kundi la msaada kwa Syria, linaloundwa na nchi 23 na mashirika yanayohusika katika viwango tofauti katika mgogoro unaonedelea nchini humo, umeshindwa kufikia ufumbuzi. Mkataba wa usitishwaji wa mapigano uliyoanzishwa na Urusi pamoja na Marekani, wiki mbili zilizopita, haukuweza kutekelezwa.

Wakati ambapo Mawaziri wa Mambo ya Nje wa kutoka nchi hizo wamekua wakikutana kwa mazungumzo mjini New York, mabomu yamekua yakidondoshwa katika mji wa Aleppo na hivyo kuoneka kuwa jumuiya ya kimataifa imeshindwa kupatia ufumbuzi hali ya machafuko inayoendelea kusuhudiwa nchini Syria.

Baada ya masaa mawili ya majadiliano, kundi lamsaada kwa Syria limeshindwa kuafikiana. Staffan de Mistura, Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria amesema ulikua mkutano uliyodumu muda mrefu, ngumu, na walishindwa kuafikia baadhi ya mambo.

Mkutano huo unaendana na tangazo la serikali ya Syria lakuanza upya mashambulizi makali katika jimbo la Aleppo. Urusi na Marekani kutupiana lawama juu ya kushindwa kwa mkataba wa usitishwaji wa mapigano kati ya serikali ya Syria na waasi.

Wakati huo huo jeshi la Syria limetangaza kuwepo kwa mapigano mapya, katika hali ya kurejesha katika himaya yake eneo linalodhibitiwa na waasi katika jimbo la Aleppo. Takriban watu laki mbili na nusu wamezingirwa mpaka sasa katika jimbo la Aleppo.

Jeshi la Syria limebaini kwamba barabara za kutoka katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi kwa sasa zimewekwa wazi ili kuruhusu watu kuondoka katika maeno hayo.

Hata hivyo jeshi pia limewatolea wito raia kujiepusha kuwa katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi.

Marekani na Urusi wameshindwa kuafikiana jinsi ya kuufufua upya mkataba wa kusitisha mapigano, nchini Syria.

Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani John Kerry alikutana kwa mazungumzo na mwezanke wa Urusi mjini New York, lakini Bw Kerry amesema Urusi inatakiwa kuonesha nia njema ya kumaliza machafuko yanayoendelea nchini Syria.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments