Hali tata yazuka kati ya Askofu Mbonyintege na Padri Ubald

Padri Ubald Rugirangoga
Kumekuwa uhasama kimya bila matatitzo au hewa isio ya kawaida, Kanisa ya kikatoliki haijawahi kufurahishwa na jinsi Kasisi Ubald Rugiragonga anavyoendelea kuvutia wengi wakitaka swala la uponyaji.

Umati wa watu husafiri kutoka kila kona za nchi kwenda popote Ubald anapoenda kufanya misa kwani wao wanataka kupona ugonjwa na kujionea jinsi anavyochapa maajabu ana kwa ana.

Kasisi Ubald anafanya majukumu katika Dayosisi ya Cyangugu ingawa anapenda kualikwa katika dayosesi mbalimbali kwa kuongoza misa ; kwa ujumla ni padri maarufu nchini kote.

Lakini, kasisi huyo yuko hatarini baada ya kutoelewana na Askofu Simargide Mbonyintega wa dayosisi ya Kabgayi.

Akiongea na vyombo vya habari Baba Ubald alisema kwamba mara moja alialikwa na watawa wa dayosisi ya Kabgayi bali Mbonyintege alikataa wao kumkaribisha katika dayosisi kwake.

‘’nilialikwa na watawa katika Dayosisi ya Kabgayi kwa kusali, kisha waliniambia kwamba askofu Mbonyintege alikataa ombi lao kutokana na sababu mimi sitaki kujua.’’ Ubald alisema.

Padri Ubald anasema kwamba huu ni wakati ngumu katika safari yake ya kiinjili,
‘’nimekuwa tayari kwa hali hii ambapo watu hawatakupenda nini ninavyofanya, lakini mimi siwezi kukata tama kwani huu ni mpango wa mungu.’’

Hata hivyo Ubald hakukukemea uamuzi wa Mbonyintege wa kumzuia kuingia katika dayosisi,

‘’ kitu muhimu ni kwamba mimi sina tatizo lolote na wakristo, muda utafika nae aelewe umuhimu wa neema ya mungu.’’ Ubald aliambia mwanahabari.

Yeye anajiona kama mtu anaye mengi ya kufanya zaidi ya kueleza umahiri wa neema za mungu, ‘’muda wao utafika na wao watajua’’ alisisitiza.

Katika mahojiano maalum na KTPress, Askofu Smargide Mbonyintege alikanusha kumzuia kuja kusali.
‘’hakuna sababu hata moja ambayo inaweza kunisukuma kwa kumzuia Padre Ubald kuitembelea Dayosisi ya Kabgayi.’’

‘’Hapana, sijui jambo hilo, linasikika mpya masikioni yangu .’’ alikana.

Mtu wa ndani mwa Dini ya Katoliki aliambia gazeti la KTPress utata huo unachukuliwa kama hatua ya mgawanyiko wa itikadi ya kikatoliki.

‘’ linawezekana kuwa hili ni swala la kisiasa kuliko swala la kidini kwani sababu yeye (Ubald) anahubiri msamaha na maridhiano.’’

Mtu huyo aliongeza kwamba Vatican ilituma barua inayotaka Ubald na wengine wa aina yake kuacha kuchanganya injili ya mungu na siasa.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments