Rwanda kuvuna maradufu mazao ya asali ya nyuki mwaka 2020.

1

Wizara ya kilimo na mifugo inasema kwamba Rwanda huvuna tani nne kila mwaka lakini wao wanapanga kutumua nguvu ziwezekanazo ili kuvuna tani nane mwaka 2020.
Dkt Mukeshimana Geraldine, waziri wa kilimo na mifugo nchini Rwanda, aliyasema wakati alipokuwa kuzindua maonyesho kiafrika ya asali (ApiExpoAfrca 2016) yanayofanyika mjini Kigali tangu 21-26, Septemba, 2016.

Dkt Mukeshimana alifunguka kuwa Rwanda inalenga wafugaji wa nyuki kubadili namna ya kufuga kwa kuimarisha taaluma kiubunifu ili kuvutia wawekezaji.

‘’tunataka kutumia teknolojia kwa kufuga nyuki ili kuachana na ufugaji wa asili, kutumia ubunifu na kuvutia wawekezaji na kukua maendeleo ya vijiji.’’ Geraldine alisema.

Lengo la maonyesho ni kuketi pamoja kwa kujadili utaratibu unaowezekana kutumika kwa kufuga, kutengeneza asali na kugawana ujuzi kuhusu ufugaji wa nyuki.

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

Tumia Comments