Gatsibo : Majambazi 88 waoneshwa hadharani.

Kwa ajili ya uongozi wa jimbo la mashariki mwa Rwanda kuonyesha yalio fikiwa kwa ajili ya kushughulikia swala la majambazi wanaoiba ng’ombe, jumatano, 21, 20116, uongozi jimbo la mashariki waonesha hadharani watu 88 wanaoshukiwa wizi hasa katika wilaya za Nyagatare, Gatsibo na Kayonza.

Tukio hilo lilifanyika kijijini Simbwa,tarafa la Kabarore, wilayani Gatstibo ambapo raia zaidi ya waliposhuhudia tukio hilo ukiongeza Francis Kaboneka, waziri wa mambo ya ndani, IGP Emmanuel K. Gasana, mkuu wa jeshi la polisi na Richard Muhumuza, mwendesha mashtaka mkuu.

Hawa 88 walikamatwa katika msako uliofanywa vijijini mbalimbali kwa ushirikiano wa raia na jeshi la polisi.

Kaboneka Francis aliambia raia kwamba yeyote anayetaka kuvunja usalama wa taifa na mipango ya maendeleo hana nafasi, hii ndio sababu viongozi katika viwango mbalimbali wanashirikiana kwa kukomesha ujambazi

‘’Rais Paul Kagame anataka nyinyi nyote kutajirika, tuungane mkono kwa kupambana na wale wanaotaka kuharibu maendeleo ya kudumu.’’ Kaboneka aliongeza.

’’’Mwezi unamalizika tukiwaahidi kupambana na wizi, leo tumekuja hapa kuwaonesha kipi tulichofanya, tunakwenda kupeleka kesi 88 mahakamani, sisi hatutakuacha kuwakamata.’’ IGP Gasana alisema.

Gasana aliwashukuru raia kwa ushirikiano waliotoa kwa kukamata hawa wizi.
Richard Muhumuza, mwendesha mashtaka wa taifa, alisema hizi kesi zitawakilishwa mahakamani moja kwa moja badala ya kupelekewa mahakama ya wapatanishi ‘ABUNZI’’

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments