Green Party yatangaza kutoridhishwa na jibu la waziri mkuu kuhusu kurekebisha sheria ya uchaguzi, karata kutupwa mahakamani.

Dkt Frank Habineza
Chama cha Demokrasia na kuhifadhi mazingira (Rwanda Democratic Green Party) kinaalalamika kutoridhishwa na jibu walilopewa na waziri mkuu kuhusu marekebisho ya ya sheria inayodhibiti uchaguzi na vyama vya kisiasa nchini Rwanda.

Katika barua waliomwandikia waziri mkuu, Green Party waliomba sheria inayodhibiti kurekebishwa ili kuruhusu vyama vyingine kupata viti bungeni, kufadhiliwa na watu kutoka nje, kuruhusa vyombo vya habari kutangaza matokeo ya kila kituo cha uchaguzi na kadhalika.

Lakini Green Party inasema kwamba maombi yao yamekataliwa na bodi ya utawala nchini Rwanda (RGB), RGB ilisema kwamba yeye haioni uzito wa ombi hilo. kwani wakati wa kupitisha sheria vyama vya kisiasa katika jukwaa lao walijadili hii sheria na Green Party hana sababu ya kulalamika, na walikosoa ombi lao kuonekana kama ni mawazi mtu pekee yake, si ombi lenye ushahidi wa kurekebisha sheria.

Hata hivyo RGB inasema kwamba iwapo vyama vinataka sheria ya uchaguzi kurekebishwa, wao ni haki yao kuketi pamoja na kulizungumzia tena.

Frank Habineza, mkurugenzi wa Green Party anasema kuwa wao hakukuridhishwa na jibu lakini wao hawawezi kukata tamaa kwani hii ndio sababu ya Green Party kuanzishwa.

Frank alisema kwamba sheria ya uchaguzi hunyima demokrasia kwa vyama vingine na kubembeleza chama tawala tu.

‘’hii ndio sababu ya Green Party kuzaliwa, kwa sababu sheria inayodhibiti vyama vya kisiasa hunyima demokrasia ili kusindikiza ukuaji wa chama kimoja tu.’’ Frank amesema.

Licha ya ombi lao kutupiliwa mabali, Green Party inasema kwamba itaendelea kujadili na wenzao katika jukwaa la vyama vya kisiasa na wanakwenda kujadili na wansheria wao kama wanaweza kuwakilisha kesi mahakamani.

Mwezi Februari, mwaka huu, wao walituma ombi hilo hilo bungeni lakini walijibiwa kwamba Bunge hana uwezo wa kuirekebisha

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments