Mataifa si mbuga za wanyama, ni watu, si miti - Rais Kagame

Rais Paul Kagame alisema kwamba kufanya mabadiliko katika jamii kunahitaji kuvuta subira, ukaweka utaratibu mpya na ukasimama imara kwa kupambana na matokeo hasi yanayoweza kutokea kuliko kubadili kila kitu.

Rais wa Rwanda ameyasema hayo jana wakati alipokuwa toa hotuba katika chuo cha Yale kilichopo mjini New Haven, katika Connecticut nchini Marekani.

Kagame aliwazungumzia watu kuhusu maendeleo ya Afrika, utawala, ukuaji wa teknolojia na mchango wake kama msingi wa mabadiliko katika ustawi wa jamii na raia wa bara la Afrika.

Yeye alisema kwamba uamuzi wa kivita ni uamuzi unaochukuliwa wakati watu wanachoka kuishi kwa kuteswa. na alibaini kwamba ni bora kuvuta subira kwa kuboresha maisha ya wananchi kuliko kuangamiza kila kitu.

‘’hatuwezi kumwaga mafuta katika takataka alafu tuwashe moto kisha tutegemee moto kufuta hayo yote kwa kujijenga baadaye . Mataifa si mbuga za wanyama ni watu , si miti.’’ Kagame alisema.

Paul Kagame alisisitiza kwamba Demokrasia ya Rwanda ina msingi kwenye yalio fikiwa na maombi ya wanyarwanda kuliko uvumi na aliongeza kuwa uhusiano kati ya viongozi na raia ni wazi na hata wao wanakutana uso kwa uso.

Haya ni matokeo ya kuheshima maombi ya raia kwani hakuna kitu kinachofanywa kinyume na maombi ya wananchi.

Baada ya kutoa hotuba katika hiki chuo, Rais wa Rwanda Paul Kagame ameandikwa kwenye orodha ya pamoja na Luis Moreno Ocampo, mwendesha mashtaka wa mahakama kimataifa ya kijinai, Mary Ribinson, aliyekuwa Rais wa Ireland na Samantha Power ambaye ni balozi wa Marekani katika umoja wataifa, Dkt Mohamed ‘’MO’’ Ibrahim, mfanyabiashara mashuhuri ulimwenguni nzima na Raila Odinga, aliyekuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Kenya.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments