Pato la Taifa kukua asilimia 5.4 – Takwimu.

Yusuf Murangwa akieleza matokeo ya GDP
Ripoti ya taasisi ya taifa ya takwimu (NISR) inatangaza kwamba pato la taifa (GDP) kukua kwa asilimia 5.4 katika msimu wa pili wa mwaka 2016 sawa na Rwf 1,549 bilioni kutoka Rwf 1,428 bilioni na kushuka katika baadhi ya sekta ukilinganisha na wa mwaka 2015.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa sekta ya kilimo ilichangia asilimia 3, huduma, asilimia 9 na utalii (hasa migahawa na mahoteli) asilimia 4 na ripoti huonyesha kuwa mapato ya viwanda alishuka hadi asilimia -2 kutoka asilimia 10 ya mwaka jana.

Yusuf Murangwa, Mkurugenzi mkuu wa NISR, amesema kwamba kushuka kumesababishwa na sekta ya migodi na ujenzi zilizo tetereka kutokana na majanga ya nje.

‘’mazao ya kilimo alikuwa kwa asilimia 4 msimu A wa mwaka 2016, mazao ya kuuza nje alishuka -23 kutokana na kushuka kwa mapato ya kahawa (asilimia -37), ingawa mapato ya chai aliongezeka kwa asilimia 4.7.’’ alisema.

Murangwa alifafanua kwamba kushuka kwa sekta ya viwanda kulisababisha matokea mabaya ya migodi na ujenzi.

‘’utendaji mbovu wa sekta ya ujenzi kulitokana na ukamilishaji wa miradi mikubwa ya ujenzi na tunatarajia matokeo mazuri ya msimu ujao.’’ Murangwa aliongeza.

‘’ ukiangalia miradi ya bomba, mabarabara yaliyojengwa katika maeneo ya vijijni, eneo maalum la viwanda,…, tunategemea ukuaji katika msimu ujao.’’ Dkt Uzziel Ndagijimana, waziri wa serikali wa mipango ya uchumi alibaini.

Ingawa uchumi katika msimu wa pili umekua polepole ukilinganisha na msimu wa kwanza ambapo asilimia ilikuwa 7.6, watalaam wa maswala ya uchumi wanasema kwamba matokeo ya sekta zilizochangia vibaya hautakuwa na athari kubwa juu ya matarajio ya ukuaji wa uchumi kwa ujumla.

Ukuaji wa uchumi wa mwaka huu unakadiriwa kuwa asilimia 6.0 mwaka huu wa 2016.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments