Waziri mkuu ajibu Green Party kuhusu mabadiliko ya sheria inayothibiti uchaguzi.

Dkt Frank Habineza, mkuu wa chama cha Green Party
Siku zilizopita Chama cha Demokrasia na kutetea mazingira kilimwandikia barua waziri mkuu Anastase Murekezi wakimuomba kurekebisha sheria inayodhibiti uchaguzi nchini Rwanda.

Akihojiwa na makuruki, Frank Habineza, mkuu wa Democratic Green Party of Rwanda amethibitisha kwamba walijibiwa ingawa amekataa kusema ni nini wao walijibiwa.

‘’ ndio, walijibu, lakini hatuwezi kutangaza jibu walitupa, tutalitangaza rasmi kesho kwa sababu bado tunalijadili.’’
Frank Habineza amesema.

Green Party alimwandikia Murekezi wakimuomba kurekebisha sheria inayodhibiti uchaguzi.

DGR wanalalamika mengi yakiwemo vyama vyote vya kisiasa kuruhusiwa kuwakilishwa katika tume ya uchaguzi, kuanzisha teknolojia kwa kupiga kura na kuruhusu vyombo vya habari kutangaza matokeo amabyo yalioneka kila kituo uchaguzi, kupungua matokeo anayohitajika kwa chama cha kisisasa kupata ushindi kutoka 5% kwa 4% na mgombea huru 2%.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments