Warundi 260 kusaidiwa kuendelea masomo yao katika vyuo nchini Rwanda

Warundi 260 waliokimbilia nchini Rwanda baada ya ghasia za kisiasa kuibuka nchini kwao wanaenda kuendelea masomo yao katika vyuo nchini Rwanda.

Wao wamekuwa 277 wanaohitaji kuendelea masomo yao lakini 270 ndio wamepata nafasi ya kuendelea masomo yao. Hawa waliobaki ni kwa sababu nyingi zikiwemo kuwa ni wajawazito au wana watoto wachanga.

Kwa hisani ya serikali ya Rwanda na shirika la Maison Shalom, wanfunzi wamepewa vifaa vya shule na kwenda kusoma katika vyuo vikiwemo UTB, UNILAK , INES Ruhengeri na Chuo cha Kibungo.

Kiongozi wa shirika la hawa wanafunzi wanaoishi kambi ya wakimbizi iliyopo Mahama, Mashariki mwa Rwanda , Jean Claude Ciza hivi karibuni aliambia Redio RPA kwamba wanashukuru serikali ya Rwanda.

‘’ tunaishukuru serikali ya Rwanda, tumejifunza kiingereza katika miezi mitatu tangu mwezi Machi, maandalizi ya kwenda chuoni anafika tamati kwa ushirikiano na serikali ya Rwanda, Maison Shalom na shirika la wakimbizi Duniani. Wanatupa vifaa vya shule vikiwemo nguo, magodoro, masabuni, viatu,….’’ Jean Claude ameiambia RPA.

Hawa wanafunzi wanasema kwamba huu ni msaada muhimu kwani baada ya kumaliza masomo wataweza kujitafutia ajira.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments