Mushikiwabo akutana na mwenzake nchini Kanada

Mushikiwabo Louise akiwa na Stephane Dion, waziri wa mambo ya kigeni nchini Kanada

Waziri wa Mashauri ya kigeni na ushirikiano, pia msemaji wa Serikali ya Rwanda, Louise Mushikiwabo amefanya mazungumzo ya kipekee na mwenzake wa Kanada, Stephane Dion.

Mazungumzo yao alilinga maswala ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili, usalama, afya na mabadiliko ya anga.

Louise Mushikiwabo yuko nchini Kanada ambapo alipokwenda kuhudhuria mkutano wa tano ulioandaliwa na shirika la Global Fund kwa ajili ya kukusanya pesa zitakazotumika katika shughuli za kupambana na virusi vya ukimwi, Malaria na kifua kikuu.

Mjini Montreal, Bi Mushikiwabo alihudhuria kongamano la wanawake wa Rwanda wanaoishi katika nchi za ugenini, Rwanda women Convention 2016.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments