Kenya na Somalia kukutana ICJ Heague kesho Jumatatu

Mwanasheria mkuu wa Kenya Githu Muigairfi
Nchi ya Kenya hapo kesho inaanza mapambano ya haki huko Hague, Uholanzi, kupambana dhidi ya madai ya kuchukua sehemu ya eneo la bahari ya Somalia ambapo vitalu vitatu vya mafuta vinapatikana.

Wakati huu, mapambano hayo yatakuwa katika jengo la kihistoria la amani ambako Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), ambayo inasikiliza kesi hiyo inapatikana likiwa umbali mdogo kutoka Mahakama ya Kimataifa ya uhalivu wa kivita ICC.

Waziri wa Mambo ya Nje na Uwekezaji wa Somalia Abdirahman Dualeh alifungua kesi kuhusu mgogoro huo tarehe 28 mwezi Agosti,mwaka 2014 kwa niaba ya serikali ya Somalia.

Mwanasheria Mkuu wa Kenya Githu Muigai ataiongoza timu ya utetezi nchini Kenya ambayo inamjumuisha mwanasheria wa Uingereza Karim Khan ambaye alimwakilisha Naibu Rais William Ruto katika mahakama ya ICC huku Somalia ikiwakilishwa na wanasheria kutoka New York na Ufaransa.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments