Wapiganaji 38 wa Boko Haram wauawa Niger

1

Jeshi la Nigeria linasema wanajeshi wake pamoja na wale kutoka Chad, wamewauwa wapiganaji 38 wa Boko Haram, kusini mashariki mwa Niger.

Jeshi linasema silaha nyingi zilipatikana katika operesheni hiyo. Boko Haram ilianza Nigeria, lakini inazidi kutapakaa katika nchi jirani.

Mapambano ya kundi hilo, yamefanya watu kama milioni mbili na nusu kukimbia makwao.

Kikosi cha kimataifa, chenye wanajeshi wa Nigeria, Niger, Chad na Cameroon, kinaongoza operesheni dhidi ya Boko Haram.

Chanzo : BBC

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

Tumia Comments