Rais Kagame kuongea juu ya utu na utamaduni wa wanyarwanda

Rais wa jamhuri ya Rwanda Paul Kagame atahudhuria tukio lililoitwa “Rwanda Cultural Day” litakalohudhuriwa na wanyarwanda na marafiki wa rwanda jijini San Francisco tarehe 24 Semptemba 2016 kama inavyoonekana kwenye mtandao wa Rwandaday.

Siku zilizopita rais Kagame aliambia vijana kwamba kinachojumuisha na kuwaunganisha wanyarwanda ni utamaduni na ndiyo maana ya majukumu ya kujiendeleza wewe mwenyewe bila kusahau majukumu unayopewa na kushiriki katika maendeleo ya wakazi wa nchi na kushirikiana katika utamaduni kama kitambulisho cha wanyarwanda.

Katika kipindi kilichorishwa hewani na redio ya taifa waziri wa michezo na utamaduni Uwacu Julienne alisema “Ni siku njema ya kukumbukwa na wanyarwanda, nadhani kuwa wanyarwanda waliisubiri kwa hamu vijana na wazee, wasomi na wasiokusoma, tajiri na wasiojiweza. La muhimu ni kuwa tunaunganishwa na utamaduni, ndiyo maana tunasema kwamba ni siku kuu yenye thamani kubwa”

Katibu mtendaji wa Rwanda Academy of Language and Culture (RALC) Dkt Vuningoma James anaunga mkono waziri Uwacu na kukubali kwamba ingawa ni ndani ama nje ya nchi, utamaduni huendelea kuwa utamaduni yaani ukatenganishwa na wakazi wao siku nenda rudi.

“Adabu ya wanyarwanda, chakula na mavazi. Hivyo ni vitu vinavyokutenganisha na ung’ambo, utamaduni unabadilika kufuatana na wakati lakini hauwezi kuzima. Sisi wanyarwanda tumebahatika kurudi kwenye chanzo”. Vuningoma.

Katika tukio hilo kutakuwepo waimbaji mbalimbali kama Masamba Intore, Mariya Yohana, Teta Diana, Mighty Popo, Muyango, King James pamoja na Urukerereza. Pia wasanii wazalendo ambao huishi Marekani watashiriki katika tukio hilo kama Alpha Rwirangira na Meddy Ngabo.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments