Kayonza : Washukiwa wa wizi wa ng’ombe 10 wakamatwa na jeshi la polisi

Jeshi la polisi wilayani Kayonza limeshika watu 3 ambao wanashtakiwa kuiba ng’ombe 10 ambao inadaiwa kwamba ng’ombe hao waliwaiba wilayani Nyagatare usiku wa kuamkia tarehe 14 Semptemba.

Wanaume hao ambao inadaiwa kwamba waliwaiba ng’ombe hao katika kata ya Karangazi na kutiwa nguvuni na ngazi za usalama katika kata ya Gahini wilayani Kayonza tarehe 15 Semptemba.

Msemaji wa jeshi la polisi mkoani Mashariki mwa Rwanda, Inspector of Police (IP) Emmanuel Kayigi alisema "Waliwapeleka ng’ombe hao kwa muuzaji wa ng’ombe aishie katika kata ya Gahini. Baada ya hayo alisikitika na kuamua kuambia jeshi la polisi iliyokaribu nae”.

“Utajiri unaopitia katika njia panya za kinyume na sheria ni mojawapo ya sababu za watu kuingia katika wizi. Watu hupaswa kuachana na wizi bali wanapaswa kupitia njia ya kujiendeleza bila kujitia matatani”. Kayigi alisema.

“Kulinda usalama wakati wa usiku ni mojawapo ya kukomesha na kusimamisha uhalifu. Jeshi la polisi linashirikiana na wananchi katika usalama wa kudumu”. Aliongeza Kayigi

Mhatia wa wizi huhukumiwa na sharia katika katiba ya Rwanda kwa kifungo cha kati ya miezi 6 hadi miaka 2 na faini ya fedha mara mbili hadi tano ya thamani ya mali iliyoibwa kama inavyonukuliwa na ibara ya 300.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments