Achana na mateso ya mapenzi !

1

Mpendwa, mahusiano yako yakoje ? Ni furaha, vicheko, upendo na starehe kwa kwenda mbele au hivyo kwako ni msamiati mkuu ? Maisha yako ni starehe ? Maisha yako ya kimapenzi ni raha au karaha ?

Aina ya mapenzi ya marafiki zetu wengi ni ya huzuni kama si ya kusikitisha kabisa. Kila siku wao ni vilio tu. Kila siku ni kushika tama. Amani na furaha wamebaki kusikia kutoka kwa wengine. Tunahitaji furaha na amani katika maisha yetu, ili tuweze kufurahia maisha na kufanya mambo bora zaidi.

Ukweli ulio wazi ni kwamba mtu akupendaye kwa dhati ni lazima apende kukuona ukiwa na furaha. Hata siku moja hatopenda kukuona ukitoa machozi. Labda ya furaha ! Mtu akupendaye mara zote hupenda kuliona tabasamu lako. Hupenda kukuona ukifurahia maisha. Ikiwa hauko na mtu mwenye sifa hizo ni wajibu wako sasa wa kujiuliza.

Kama unapendwa au unafanywa chombo cha starehe, au mtatuzi wa shida zake, hasa za kipesa. Ila kuna idadi kubwa ya watu ambao wako katika mahusiano na watu ambao hawawapendi kwa dhati japo hawataki kuwatamkia mdomoni. Kutokana na hali hiyo hushindwa kujizuia kuwakera ama kuwaumiza. Mara nyingi huwasababishia majuto.

Taratibu hamu na wapenzi wao huanza kuwatoka. Wachache huamua kuachana nao, ila wengi huwa hawana ujasiri huo. Ndugu yangu, hali ya mahusiano yako ikoje ? Kwanini bado unaendelea ‘kupigika’ katika mahusiano ya namna hii ?

Kweli uamuzi wa kuachana na mtu unayempenda ni mgumu sana. Ila jiulize, maisha hayo mpaka lini ! Maisha ya kuendelea kumlilia mtu asiyetambua thamani ya chozi lako. Mtu asiyekupenda. Zinduka rafiki. Hakuna utakachokipata huko zaidi ya majonzi na manung’uniko yasiyoisha.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

  1. nikweli ni ngumu kumuacha mtu umpendae ila inapozidi unakaza moyo na kuachan nae mapenzi yanaumiza asikwambie mtu

Tumia Comments