Rais Kagame anasubiriwa nchini Marekani

Rais Paul Kagame anasubiriwa nchini Marekani ambapo atahotubu katika chuo cha Yale kilichopo mjini Connectcut Mwezi Septemba 24, mwaka huu katika tukio la Coca-Cola World Fund Lecture ndani ya ukumbi wa Henry R. Luce.

Ni dakika chache tu kabla ya tukio litakalojumuisha wanyarwanda na marafiki zao ‘’Rwanda Cultural day’’ mjini San Francisco, tarehe 24.

Yale University ilianzisha tukio hilo katika mwaka wa 1992 kwa lengo la kuisaidia miradi mbalimbali ya watalaam wa maswala ya ushirikiano, sheria ya kimataifa, …
Hotuba ya Paul Kagame itawavutia waalimu, wafanyakazi wa chuo na wengine kutoka ndani na nje ya Marekani.

Katika hiki Chuo cha Yale, Kagame anasifiwa utawala wake bora, hasa mchago wake wa kurejesha amani, umoja na upatanishi kati ya wananchi , kutetea haki za kibinaadamu na kuboresha maisha ya wanawake.

Yale University inasema kwamba ilimwalika Kagame kwa ajili ya kuwazungumzia wamarekani na wageni maswala mbalimbali yakiwemo maendeleo ya Afrika, utawala, na umuhimu wa teknolojia kwa kuboresha ustawi wa waafrika.

Akitoa hii hotuba, Kagame atabainika kuwa ni miongoni mwa watu mashuhuri duniani kama Moreno Ocampo, aliyekuwa mwendesha mashtaka wa ICC, Mary Robinson, aliyekuwa Rais wa Ireland, Samantha Power, balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa, Dkt Mohamed ‘’MO’’ Ibrahim na Raila Odinga, aliyekuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Kenya waliotoa hotuba katika tukia hilo,...

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments