“Sisi katika RPF tunajiita familia, kutuita chama ni kuzidi’’- Seneta Tito

1

“Seneta Tito Rutaremara ,pia ni mwanachama wa chama tawala RPF-INKOTANYI, anasema kwamba RPF ni familia inayounganisha wanyarwanda kusema ni chama, ni kama kusema Tito ni Joseph."

Katika kipindi kilichorushwa hewani na Redio Flash FM leo asubuhi kuhusu Demokrasia, Seneta Tito Rutaremara amesema kwamba RPF inaitwa familia kama walivyoamua na hakuna sababu ya kusema kwamba ni chama na inamaana ya kuwa hakuna mtu mwenye haki ya kubadilisha jina hilo.

“Hayo ni makosa ya kutovumilia wakati mnaposema kwamba ni chama, ingawa nimeitwa Tito hamna budi ya kuniita jina lingine . Tumejiita familia, tunawaomba kutuita kama hivyo, mkitaka maelezo zaidi tutawafafanulia kinaghaubaga”. Seneta Tito alisema.

Katika mahojiano na Claude Ntezimana katibu mkuu wa Democratic Green Party waliongea juu wanasiasa hupaswa kushirikiana na kuwa huru ya kusema na kujilinda maneno ya kutenganisha wananchi.

“Haki ya kusema kuwa watu wauwane, wale wasemayo hayo wana lengo maalumu kwa nchi zao, mkazi wa nchi hiyo anasema kwamba ataenda kumtafuta rais wa nchi fulani na kumpiga makofi na kumpereka gerezani, sijawahi kusikia kuwa alitenda kinyume na sheria”. Seneta Tito aliongeza.

Katibu mkuu wa Green Party Ntezimana alisema “Wanasiasa wanaifahamu ubaguzi, kwa usasa hakuna mtu apaswae kujitia matatani hayo, hatuwezi kuvumilia mtu anayesema maneno ya ubaguzi lakini watu wanaosema kuwa hawana uhuru wa kimedokrasia hawapaswi kushukiwa ubaguzi. Wanyarwa tumeishaelewa ubaya wa ubaguzi ndiyo maana tunawahamasisha kuachana na mawazo hayo”.

Lengo kuu la familia ya RPF INKOTANYI ni kukomboa mnyarwanda katika hali umaskini, ubaguzi na siasa mbaya ya unyanyasaji wa haki ya binadamu na kuwa huru katika umoja, demokrasia na maendeleo ya kudumu.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

Tumia Comments