Meja Rugomwa ahukumiwa siku thelathini jela

Hakimu wa mahakama ya kijeshi iliyopo Wilayani Nyarugenge, mjini Kigali amemhukumu Meja, Dkt Rugomwa Aimable na Nsanzimfura Mamerito siku thelethini jela baada ya kesi dhidi yao kusikilizwa.

Wao wanashtakiwa kumuua Theogene Mbarushimana ,18, wakimpiga hadi kufa baada ya kumkamata akilala chini ya gari Meja Rugomwa wakisema ni mwizi.

Mahakamani, Meja Rugomwa aliomba kuachiwa kwani yeye alishambuliwa nyumbani lakini Hakimu amepuuza hivyo, Mahakama imesema kuwa marehemu alipigwa kitu kichwani, kuwa wapo mashuhuda waliojionea RUgomwa akimpiga mtoto, kuwa vipimo vya mganga vinaonesha kwamba marehekemu alipigwa na kukatwa vidole viwili hizi ndizo sababu kubwa za kumfunga meja na mwenzake siku thelathini gerezani kabla ya kufunguliwa mashtaka kwa kina.

Mawakili wao wamesema kuwa hawakubali matokeo ya mganga kwani yeye hana uwezo. Linalomhusu Nsanzimfura, mawakili wamesema kwamba yeye ana tatizo la akili kwa hivyo yeye anastahili uhuru lakini mahakama imekataa sababu hiyo kwani hakuna nyaraka za mganga zinazoonesha kwamba Nsanzimfura ana tatizo hilo.

Meja Dkt Rugomwa Aimable amekuwa mganga wa hospitali ya kijeshi iliyopo Kanombe, Wilayani Kicukiro.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments