Gasabo : Wafanyakazi wa kiwanda cha nguo wameandamana.

Wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha S*H kinachomilikiwa na wachina wameandamana katika saa za asubuhi ya leo.

Hawa wafanyakazi takriban 200 wamekuwa wakisema kwamba wao hawawezi kurudi kazini kama vilivyokuwa bila kulipwa mshahara waliokubaliana na mamlaka ya masomo ya ufundi.

Mmoja wao aliyeongea na makuruki.rw amesema kwamba wafanyakazi ambao wana tatizo hilo ni angalua mia tatu.

Hawa ni wafanyakazi waliotumwa na WDA(Mamalaka ya masomo ya ufundi) kwa ajili ya kushiriki kwa kuongeza uzalishaji wa hiki kiwanda. Wao wanasema kuwa wamekubaliana kulipwa Rwf 45, 000, ukiondoa Rwf 5,000 ya chakula lakini wanalalamika kwamba wameshangazwa na kulipwa kiasi kidogo (Rwf 5000 au Rwf 10,000) ukilinganisha na mshahara waliokubaliana.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments