Maandalizi ya mbio za baiskeli yaanza.

Gasore Hategeka
Chama cha baiskeli Rwanda FERWACY kinasema kwamba wachezaji zaidi ya 18 kutoka ndani wapo katika mafunzo mkali kwa ajili ya kijiandaa mbio za baiskeli TOUR DU Rwanda zinazotarajiwa kufanyika nchini Rwanda mwezi Novemba,13-20. Mwaka huu.

Katibu kudumu wa FRWACY Emmanuel Murenzi anasema kuwa Rwanda itakuwa ikiwakilishwa na timu moja ya taifa na klabu mbili ambazo ni klabu Benediction ya Rubavu na Friends of Rwamagana Sports Club. Hapo awali Rwanda ilikuwa ikiwakilishwa na timu tatu za kitaifa(Akagera, Muhabura na Karisimbi), FERWACY inasema hii ni kwa lengo la kuzisaidia timu nyingine kuboresha uwezo wao.

‘’tunakwenda kuandaa wanaspoti vizuri kabla ya mashindano, tunataka wajue ni nini nchi inatarajia kwao.’’Murenzi amesema.

Tour du Rwanda ya mwaka jana ilinyakuliwa na Jean Bosco Ndayisenga wakati mbio za awali Valens Ndayisenda aliibuka kidedea.

Haya mashindano ya baiskeli yanajumuisha timu nyingi zikiwemo timu ya taifa ya Afrika kusini, ya Ethiopia, Eritrea, Misri na Algeria na klabu kama Dimension Data For Qhubeka (South-Africa), Kenyan Riders Downunder (Kenya), Sharjah Cycling Team (United Arab Emirates), Cycling Academy Team (Israel) Tirol Cycling Team (Austria), Stradalli Bike Aid (Germany), Lowestrates.Com (Canada), Team Haute-Savoie Rhone-Alpes (France) and Team Furniture Decarte (Switzerland).

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments