Bunge la EAC kufanya utafiti kuhusu mauaji ya halaiki dhidi ya Watutsi

Wageni wakisoma ujumbe kwenye kuta katika makumbusho ya mauaji ya kimabri, Gisozi
Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EALA) limeunda na kutuma kamati ya kufanya utafiti kuhusu mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda katika mwaka wa 1994 dhidi ya jamii ya Kitutsi. Hii kamati inatarajia kuchunguza jambo la mauaji ya kimbari na kiwango cha itikadi ya mauaji ya kimbari katika kanda.

Bodi Odiko, mjibika wa mahusiano ya umma, anasema kwamba hii kamati ya watu tisa ambayo inaongozwa na Mkenya Mbunge wa EALA Judith Pareno, ilichaguliwa katika kikao cha wabunge kilichofanyika mjini Arusha, Tanzania na wanatarajiwa kutembelea mataifa wanachama wa EAC na wadau.

Mbunge Martin Ngonga ambaye yupo katika kamati hiyo anasema kuwa wana miezi mitatu ya kufanya utafiti na kutoa ripoti kwa wabunge.

‘’ ni kitu muhimu sana katika kazi ya bunge, suala la mauaji ya halaiki na kuyakana ni jambo haliwezi kufumbiwa macho tu na watunga sera, hii ni ukweli katika hii kanda yetu.’’
Ngonga amesema.

‘’kwa makusudi na madhumuni, hatuwezi kukubali huu mwenendo, hii ndio maana tunapaswa kuweka mikakati na utaratibu kwa kutokomeza ukiukaji wa haki za binadamu. Kitu ambacho bunge linakwenda kufanya sio mwisho, itakuwa kawaida.’’
Ngoga amesisitiza.

Huu utafiti amabyo unatarajiwa kufanywa mjini Kigali wiki, ni kutokana na wazo liliotolewa na Mbunge Abubakar Ogle anayewakilisha Kenya na kupitishwa na wabunge mwaka jana.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments