DRC : Wajumbe wa upinzani wajiondoa katika mazungumzo

Rais wa chama cha UNC, Vital Kamerhe, akihojiwa na vyombo vya habari wakati wa ufunguzi wa mazungumzo. Ni msimamizi msaidizi wa mazungumzo kutoka upande wa upinzani unaoshiriki mazungumzo hayo.

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ujumbe wa upinzani umesitisha ushiriki wake katika mazungumzo wa kitaifa, mazungumzo yaliyoombwa na Rais Joseph Kabila kwa minajili ya kujiandaa uchaguzi ujao. Tangazo ambalo si mshangao.

Kiongozi wa ujumbe wa upinzani Vital Kamerhe ndiye alitangaza uamuzi huo alipokua akiondoka katika tume pana inayosimamia mazungumzo hayo. Tume ya uchaguzi itajadili kalenda ya uchaguzi na daftari la uchaguzi, masuala mawili muhimu katikal mazungumzo hayo.

Ujumbe wa upinzani ulionya kwamba kuna mistari nyekundu haitakiwi kuvukwa, hasa uchaguzi wa urais na wa wabunge unapaswa kupangwa katika nafasi ya kwanza. Inafahamika kwamba chama tawala na vyama vinavyokiunga mkono wana maoni tofauti na wanabaini kwamba uchaguzi wa serikali za mitaa ndio unapaswa kufanyika, kwa hiyo itakua ni kurudi nyuma na kwamba sio lazima kuachana na uchaguzi huu.

Wito kwa jumuiya ya kimataifa

Kwa upande wake Vital Kamerhe, kiongozi wa chama cha UNC na kiongozi wa ujumbe wa upinzani, anasema jukumu kwa kushindwa kuandaa uchaguzi ni kutokana na serikali. Hata hivyo, azimio 22-77 limekua likitoa kipaumbele kwa uchaguzi wa urais, na ule wa wabunge, na inatakiwa jumuiya ya kimataifa kuheshimu maandiko ambayo ni muhimu katika mazungumzo haya, yaani Katiba, azimio 22- 77 na Mkataba wa Umoja wa Afrika.

Serikali na vyama vinavyoiunga mkono wanasema tume ya usuluhishi inatakiwa ifanye kazi yake vilivyo. Kila upande umekua ukitoa msimamo wake. Kambi hiyo inajiuliza iwapo tume ya usuluhishi utachagua kutumia azimio 22-77 na makubaliano ya wote.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments