Wanasiasa na wanajeshi wanufaika na vita Sudan Kusini

Rais Kiir na Riek Machar walibuni serikali ya umoja mwaka huu lakini kwa sasa Machar ametimuliwa.

Wanasiasa pamoja na wakuu wa jeshi nchini Sudan Kusini wanaripotiwa kujitajirisha wakati nchi hiyo imepoendelea kukumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kulingana na ripoti ya shirika la Sentry linalofadhiliwa na muigizaji George Clooney pamoja na mwanaharakati John Prendergast.

Waandishi wa ripoti hiyo yenye kichwa,Uhalifu wa Vita Haustahili Kulipa, walisema kuwa walichunguza uhusiano uliopo kati ya wakuu nchini Sudan Kusini na pesa zilizonunua nyumba za kifahari na biashara nyingi za madini, mafuta na za kifedha.

Shirika la Sentry linawalaumu Rais Salva Kiir, kiongozi wa upinzani Riek Machar na majenerali wakuu jeshini pamoja na familia zao kwa kunufaika wakati mamilioni ya watu nchini humo wamekuwa wakitaabika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Tofauti za wanasiasa waku wawili zilisababisha kutokea mapigano yaliyozuka mwezi Disemba mwaka 2013.

Ripoti moja ilisema kuwa , inaonekana watu wachache wanadhibiti asilimia kubwa ya uchumi wa Sudan Kusini na wengi wa watu hawa ni wale walio madarakani.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments