Mufti Hitimana awaomba waislamu kuzuia watoto wao kujiunga na makundi ya ugaidi.

Hitimana ameyasema hayo katika ibada ya sikukuu ya Eidd Al-Hajj iliyofanyika uwanjani wa Kigali/Nyamirambo.

Jumatatu hii Waislamu duniani kote wanasherehekea sikukuu ya Idd El Hajj wakiungana na wale (Mahujaji) walioko katika miji ya Makkah na Madina, nchini Saudi Arabia wakiendesha ibada mbalimbali.

Mufti Salim Hitimana amewaomba waislamu kufutilia watoto wao karibu ili kuwazuia kujiunga na makundi ya ugaidi.

‘’wazazi, mnatakiwa kuwa karibu na watoto wenu kwa kujua jinsi wanavyoishi ili kuwalinda kuwa na uhusiano wowote na makundi ya kigaidi.’’ Amesema.

‘’Wazazi wanahamasishwa kujua watoto wao wanafanya nini kwenye kompyuta na simu zao ili kujua hakuna mtu aneyetaka kuwafanya magaidi.’’ Aliongeza.

Mufti Hitimana anasema kwamba waislamu hawapaswi kutumia uhuru waliopewa na Rais Kagame kwa kuvunja maendeleo ya nchi.

Na amebaini kuwa wale wanaofanya vita vya kigaidi wanajiita waisalamu lakini si waislamu, ni maslahi za kipekee.

Barani Afrika sikukuu hii inasherehekea katika nchi mbalimbali, huku baadhi ya nchi zikiwa katika hali ya sintofahamu kutokana na makundi yanayodai kuwa yenye msimamo mkali wa kidini, hasa nchini Somalia, Nigeria, Mali, Libya, Mauritania na nchi nyingine za Kiarabu barani Asia, na Ulaya.

Kati ya Waislamu duniani sikukuu hii hujulikana kwa majina mbalimbali ambayo hutafsiriwa pia kwa lugha mbalimbali kama vile :
Idd-al-Adhha yaani sikukuu ya sadaka

Idd-al-Qorban sikukuu ya sadaka (kwa kutumia neno tofauti ya "sadaka" katika Qurani) ; Kituruki : Kurban Bayramı ; Kikurdi "Cejna Kûrbanê" ;

Idd-al-Kabir au "sikukuu kubwa" ; "Bari Eid" huko Uhindi na Pakistan ; jina hili hutumiwa kwa sababu kati ya sikukuu mbili zinazoamriwa katika Qurani hii ni sikukuu kubwa zaidi.

Kila Muislamu mwenye uwezo hupaswa kumchinja mnyama wa sadaka siku hiyo mara nyingi kondoo lakini kuna pia sadaka za mbuzi, ng’ombe au ngamia kufuatana na uwezo na kawaida ya nchi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments