’’Hatutakubali nchi yetu kupita kama takataka’’, Kagame awaambia vijana

Rais Pual Kagame ameyasema haya maneno wakati alipokuwa akikamilisha ITORERO INTAGAMBARUZWA II ambalo lilijumuisha wanafunzi wa vyuo.

Katika hii sherehe iliyofanyika katika jengo la Kigali convention center ,mkuu wa taifa la Rwanda aliwahimiza vijana kuzingatia utamaduni wa umoja, uwajibikaji na kufikiri kubwa ili kuhakikisha kuwa nchi inaendelea kufikia malengo yake ya mabadiliko kiuchumi ya jamii.

Haya masomo ya jamii yalijumuisha wanafunzi zaidi ya 2,000 kutoka vyuo binafsi na umma kwa ajili ya kujifunza mambo ya uzalendo na ujasiriamali na kadhalika.

Mkuu wa Taifa aliwahimiza wanafunzi kufikia kubwa kwa kufikia matarajio yao na kufanya kazi na bidii ili kutimiza ndoto.

‘’Nchi yetu inaweza kuwa ndogo lakini watu wetu wanapaswa kufikiri kubwa, mawazo hawana mipaka.’’ Rais Kagame alisema.

‘’hatutakubali nchi hii kwenda bila mpango, nguvu za kufikiri na ujuzi wa vijana katika chumba hiki na nchini kote hawawezi kupita kama taka taka. Hatutaki kuwa nchi iliyopoteza uwezo na ujuzi.’’
Aliongeza.

Kagame alibaini kwamba umuhimu wa ITORERO ni kuchemsha uwezo wa kukua akili ya ubunifu na kujifunza utumadani wa uzalendo.

Kagame aliwakumbusha wanafunzi kuwa ITORERO hutumika kama fursa ya kujifunza kuwa umoja ni msingi muhimu kwa maendeleo endelevu na kutoa wito kwa washiriki kuchukua umiliki na wajibu wa kuwepo wa nchi ya siku za uso.

‘’Elimu ni moja wa utambulisho wetu lakini kitu muhimu ni nani utakuwa na jinsi ambavyo utachagua kufanya kazi.’’ Kagame aliwashauri.

Yeye alihamasisha kuonyesha maoni yao dhidi ya yeyote anayejaribu kuvunja usalama, umoja na maendeleo yaliyofikiwa katika miaka mingi iliyopita.
Eustache Ndayisaba aliyesema kwa niaba ya wanafunzi, alisema ITORERO alikuwa muhimu kwani katika ITORERO wao walijifunza namna ya kujiendeleza wenyewe na kujijengea taifa kwa ujumla.

‘’tunaahidi kufanya kazi na bidii na kufanya utafiti hasa kuhusu ICT na kilimo, tumejifunza kwamba hatupaswi kupuuza kazi yeyote, kuwa wabunifu na wajasiriamali.’’ Alisema.

Kwa mujibu wa Boniface Rucagu, mwenyekiti wa ITORERO, Haya masomo ya jamii alihudhuriwa na wanafunzi 2,090, wakiwemo wanwake 680.

Wanafunzi walioshiriki masomo ya jamii

na Jenerali James Kabarebe, waziri wa ulinzi, alishiriki sherehe ya kukamilisha ITORERO INTAGAMBURUZWA.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments