Mushikiwabo atoa salamu za rambirambi kwa Watanzania waliopoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi

Watu kumi na mmoja wamepoteza maisha na wengine mia moja na sitini na mbili kujeruhiwa kaskazini magharibi mwa Tanzania baada ya tetemeko la ardhi lenye kipimo cha richa 5.7 kupiga mkoa wa Kagera,kama jeshi la polisi nchini Tanzania lilithibitisha

Akitumia ukurasa wake wa Twitter, Louise Mushikiwabo, waziri wa mashauri ya kigeni na ushirikiano, pia msemaji wa serikali ya Rwanda ametangaza kuwa amesikitishwa na waliopoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi lililotukia jumamosi iliyopita.

‘’Pole sana kabisa #Tanzania kwa ndugu waliopoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi ! Huenda maisha akawa mazuri kwa waliojeruhiwa.’’
Mushikiwabo ameandika kweney Twitter.

Duru zinasema tetemeko hilo limeukumba pia mji wa Kampala na Rakai nchini Uganda saa 9 alasiri.

Mitetemeko mingine midogo pia ilisikika katika mataifa jirani ya Kenya Rwanda na Uganda.

Ripoti za kitaalamu zinadai tetemeko hilo limetokea katika mpaka wa Tanzania na Uganda, kilometa 47 kaskazini mwa Bukoba mkoani Kagera kufuatia mpasuko wa ardhi katika Bonde la Ufa la magharibi karibu kabisa na Ziwa Victoria.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments