Viongozi wa Afrika Mashariki na Muungano wa Ulaya wajipa miezi mitatu kabla ya kusaini makubaliano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki aliongoza mkutano wa 17 wa dharura wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afika Mashariki Ikulu jijini dar es salaam Septemba 8,2016.

Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki imeongeza miezi mitatu zaidi kuweza kusaini makubaliano ya kiuchumi kati ya Jumuiya hiyo na Jumuiya ya Ulaya kuweza kupata muda zaidi wa kuyapitia tena.

Rais wa Tanzania John Magufuli amebainisha kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki imeiomba EU kutoiadhibu Kenya ambao teyali wamesha saini mkataba huo

Tanzania na Uganda zimekuwa zikipinga mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments