#AS Kigali tournament : Rayon yampiga mtu viboko na Mkongo aonyesha nguvu.

Rayon Sports
Katika michezo ya kufungua mashindano AS Kigali Tournament yanayofanyika Rwanda, AS Vita Club ya DRC yaibamiza AS Kigali (mwandalizi wa mashindano) 1-0 uwanjani wa Kigali/Nyamirambo.

Goli la AS Vita Club lilifungwa na Oumari Sidibe kunako dakika ya 19 ya kipindi cha kwanza.

Mshambuliaji Mnyarwanda Sugira Ernest anayeichezea AS Vita Club alijaribu kufunga goli lakini yeye hakukuweza kufanikiwa na mikwaju mingi aliyojaribu.

Baada ya wao kusafisha uwanja, Rayon Sports yenye mashabiki wengi, mbwembwe, na shangwe wameshuka dimbani saa kumi na mbili na dakika kumi tu dhidi ya timu ya kipolisi.

Timu ya Rayon : Ndayishimiye Eric Bakame (nahodha), Senyange Ivan, Ishimwe Issa Zapi, Manzi Thierry, Munezero Fiston, Niyonzima Olivier, Manishimwe Djabel, Kakure Mugheni Fabrice, Mussa Camara, Lomami Frank, na Nshuti D. Savio.

Na Nzarora Marcel, Ndayishimiye Celestin, Nzeyimana, Twagizimana Fabrice, Ngendahimana Eric, Ndatimana Robert, Ngomirakiza Hegman, Usengimana Danny, Songa Issai, Uwihoreye, na Mugabo Gabriel kwa upande wa Police Fc.

Muda si mrefu, Rayon na Police walianza vita kunako dakika ya 10, Eric Ngendahimana aligonga mpira kwa kichwa kisha Bakame akasinzia, Police bao 1- Rayon Sports sahani tupu

Dakika ya 25, Rayon Sports wameamka na kufunga bao la kusawazisha lililofungwa kwa free kick ulioachwa na Savio Dominico Nshuti.

Tangu dakika hiyo mechi imechezwa kwa upya, Rayon Sports na Police wakavutana wakavutana na wakuvuuuutana kweli, katika dakika za nyongezo goli likajitokeza paa ! Huo alikuwa Bonge la mtu, bonge la Mshambuliaji Mussa Camara aliyegonga mpira kwa kichwa , kisha Rayon ikapata bao la ushindi (2-1).

Mussa Camara wa Rayon Sports

Wachezaji wa Police Fc wakisherehekea bao la kwanza

Wenzake wakimpongeza Savio baada ya kufunga bao la kusawazisha, pembeni ni Mussa aliyefunga bao la ushindi

Rwarutabura na wenzake, mashabiki wa Rayon

Masud Djouma aliambia wanahabari kwamba mechi ilikuwa hatari

Picha : umuseke.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments