Bazivamo achukua mikoba ya kuwa naibu katibu mkuu wa EAC

Christophe Bazivamo apishwa kuwa naibu katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Bazivamo alitawazwa rasmi siku ya Alhamisi ya mwezi Septemba, 08,2016 katika mkutano maalum wa marais wa nchi za EAC uliofanyika jijini Dar Es Salaam nchini TZ.

Baada ya Christophe kuchukua majukumu majukumu mapya katika jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Paul Kagame alimtakia kazi njema pamoja na workmates wake.

‘’namtakia naibu katibu mkuu kazi njema, namtakia yeye na wenzake kufanikiwa na majukumu yao. yeye anaenda kufanya kama Mwafrika wa mashariki kuliko kuwa mnyarwanda.’’ Kagame amesema.

Bazivamo alikuwa gavana wa jimbo la Gitarama( la zamani) tangu mwaka wa 1999-2000, tangu 20000- mwishoni wa mwaka wa 2002 alikuwa katibu mtendaji wa Tume ya Uchaguzi NEC.

2002-mwezi Mei,06,2011 yeye alikuwa waziri katika wizara mbalimbali zikiwemo : wizara ya mambo ya ndani, wizara ya mazingira, misitu, maji na migodi, wizara ya kilimo na ufugaji.

2011-alikuwa mbunge aliyewakilisha Rwanda katika Bunge ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Na Kati kati mwaka wa 2016 alichaguliwa kuwa naibu katibu mkuu wa EAC, na pia Bazivamo tangu 2002 ni makamu rais wa chama tawala RPF-Inkotanyi.

Bazivamo alisomea kilimo katika chuo kikuu cha Rwanda, baadaye alikwenda kusomea nchini Ujerumani katika chuo cha Göttingen ambapo alipewa Masters degree katika kilimo.

Rais Kagame amatakia Bazivamo kufanikiwa

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments