“tupunguze maneno, tuongeze vitendo kwa ajili ya kilimo.’’ – Paul KAGAME

Rais Paul Kagame anasema kwamba ni vizuri Waafrika kuachana na maneno kwa ajili ya kuimarisha kilimo kuliko kuishi kwa maneno.

Kagame ameyasema hayo katika mkutano wa siku tano kuhusu Kilimo uliowakusanya viongozi barani nchini Kenya kwa ajili ya kujadili maswala ya kilimo ( Africa Green Revolution Forum,AGRF.)

Akiwa na Rais Uhuru Kenyatta, Kagame amesisitiza kuhusu umuhimu wa kilimo ambako amesema kuwa kilimo huoneka kuwa ndogo ingawaje ni msingi mkubwa wa uchumi wa nchi.

‘’kilimo si moja ya nguzo za maendeleo yetu, ni egemeo la uchumi wetu. Fursa ambazo Afrika ina, tunapaswa kuzitumia […], tunahimizwa kuboresha kilimo na fursa zingine zinazoweza kukua uchumi wa waafrika.’’
Rais Kagame amesema

Kagame aliongeza changamoto kubwa ni kuwa kuna makubaliano ambayo anasainiwa lakini utekelezaji ukabaki katika maneno.

‘’hatupaswi kukwama katika maneno, tuendelee kusonga mbele kwa kupiga hatua tunazostahili, hebu tupunguze maneno, tuoongeze vitendo. Muda umefika kufanaya na nguvu zisizoonekana tangu zamani ili tutimize ndoto zetu.’’ Kagaem aliongeza

Huu mkutano ulivutia na watu takriban 15 na katika mkutano makubaliona ya kuimarisha kilimo anatarajiwa kufikiwa.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments