Kigali : mtu akamatwa kwa kujiita traffic police

Jeshi la Polisi limemkamata mtu aliyekuwa ajiita polisi na akawaomba raia pesa akiwaambia kwamba yeye anaweza kuwasaidia kujisajili kwa kufanya mitahani ya kupata ruhusa ya kuendesha magari.

CIP Emmanuel Kabanda ambaye ni msemaji wa polisi tawi la mtaani anasema kuwa mbadhirifu ametiwa nguvuni baada ya kudanganya watu watatu kwamba yeye ni polisi na anaweza kuwasaidia kupata nywila ambazo wanaweza kutumia kwa kujisajili kwenye mfumo wa Irembo kwa bei ya Rwf 35, 000 kila mtu.

Lakini akawapa nywila feki, baada ya kujaribu kujisajili kwenye Irembo na kushindwa wao walijuuza polisi kisha polisi wakamsaka mhalifu na kumkamata.

Mshtakiwa akikutwa na hatia ya udanganyifu, atahukumiwa kifungo cha miaka mitatu hadi mitano na adhabu ya Rwf 3 milioni hadi Rwf 5 milioni.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments