Waislamu waambiwa kuwa kutenda dhambi la ugaidi ni kama kuchanganya maziwa na damu

Sheikh Musa Fazil Harerimana, waziri wa usalama wa ndani
Katika mkutano wa usalama na waislamu wanapoishi Wilayani Rubavu, waziri wa usalama wa ndani Sheikh Musa Fazil Harerimana aliwaambia kuwa kutenda dhambi la ugaidi ni kama kuchanganya maziwa na damu.

Sheikh Fazil aliambia waislamu kwamba ndio wao wanaopaswa kuwa kwenye msatari wa mbele kwa kupambana na ugaidi kwani magaidi wanachafua dini lao.

Na yeye aliwakumbusha kwamba wanapaswa kutumia nguvu zote kwa kukomesha ugaidi nchini Rwanda kama ishara ya kutoshirikiana na wanaojiita waislamu.

Mpaka sasa utafiti ulionesha kuwa Wilaya ya Rubavu iko miongoni mwa wilaya ambazo zina watu walioambukizwa itikadi ya ugaidi.

Fazil amekutana na waislamu wa Rubavu baada ya watu watatu kuuawa wakipigwa risasi na jeshi la Polisi wakishukiwa kuwa magaidi wilayani Rusizi,magharibi mwa Rwanda.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments