Mkutano wa uwekezaji ulimwenguni unaanza mjini Kigali

Mtazamo wa angani wa eneo maalum kwa Viwada (Kigali special economic zone)

Bodi ya maendeleo Rwanda(RDB) inasema kuwa mkutano wa uwekezaji ulimwenguni unaanza leo mjini Kigali.

Huu mkutano unatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe angalau 1,000 wakiwemo wakuu wa serikali, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na wanachama wa sekta binafsi.

Francis Gatare ambaye ni mtendaji mkuu wa RDB aliliambia gazeti la The newtimes kwamba katika mkutano huo fursa na ushirikiano kutakuwa kwenye ajenda ya mazungumzo ili kuimarisha ongezeko la fursa za kuwekeza nchini Rwanda na hata barani Afrika kwa ujumla.

Global investment meet inafanyika ndani ya ukumbi wa Kigali Convention Center mjini Kigali/Rwanda.

Huu mkutano unafanyika nchini Rwanda baada ya ya kufanyika mjini London na hii ni kwa mara ya kwanza Global Investments meet kufanyika abarani Afrika.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments