‘’Sisi wanyarwanda, tunataka kujitawala wenyewe lakini haitakuwa kama zawadi kutoka nje.’’ – Kagame.

Rais Paul Kagame ameyasema hayo katika mkutano na wandishi wa habari yeye na Rais Patrice Talon wa Benin wakati alipokamilisha ziara yake ya siku tatu nchini Rwanda.

Akijibu suala la matangazaji wa RFI kuhusu mabadiliko ya katiba ya Rwanda kwa kumruhusu Kagame kuwania muhula watatu madarakani, ikiwa Kagame na Talon wote walisisitiza kuwa ni jukumu la wananchi kuweka katiba inayofanana na matarajio yao bila kuingiliwa.

Rais wa Benin, Patrice Talon amesema kuwa kufanya mabadiliko madogo ya katiba si ndio maana ya kutaka kung’ang’ania kwenye madaraka, ni kutaka kuwa na katiba sawa na maombi ya wakazi kwani akitaka kushikamana kwenye madaraka aliweza kusema aacha tuandike muhula wa miaka 15, 20 au 30.

Akimuunga mkono, Kagame amesema kwamba cha kwanza ni manufaa ya wananchi. Yeye aliongeza kuwa vyombo vya habari vya Ulaya hufungia jicho sababu ya kuwa nchi zinatofautiana kutokana na matarajio ya wananchi wa kila nchi.

Kagame alibaini kuwa wanyarwanda wanataka kujitawala wenyewe lakini haitaanguka kama zawadi.

‘’ sisi wanyarwanda, tunataka kijitawala wenyewe kama tunavyotaka lakini si jambo ambalo halitatukia kama zawadi kutoka nje ambapo nao wanapokabiliwa na matatizo ya utawala bora.’’ Kagame amesema.

Ziarani yake, Patrice Talon amesema kuwa wamesaini makubaliano ya kuimarisha biashara, utalii, viwanda vya nguo na kadhaa kati ya Rwanda na Jamhuri ya Benin.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments