Warundi wawili wapigwa risasi, Rusizi.

Wanajeshi wa Rwanda waliokuwa wakishika doria tarafani Bugarama, Wilayani Rusizi, Magharibi mwa Rwanda wamepiga risasi raia wawili wa Burundi baada ya wao kuvuka mpaka kimya kimya na kukataa kuongea na washika doria waliokuwa mpakani.

Luteni kanali Rene Ngendahimana ambaye ni msemaji wa majeshi ya Rwanda alithibitisha kuwa hawa warundi walifariki dunia katika ajali ya risasi iliyotukia huko Bugarama katika saa tisa za usiku, juzi.

Ngendahimana amesema kwamba washika doria waliwaona watu wane au watano wakivuka mpaka kisha wanajeshi wakawasimamisha ili kuongea nao lakini wao wakanyamaza, wanajeshi walikutwa na wasiwasi kisha wakaanza kufyatua risasi.

Ngendahimana amesema kwamba katika asubuhi ya Jumatano walitambua wafu ni raia wa Burundi lakini sababu iliyowafanya kuvuka mpaka haijulikani.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments