Rais Kagame afungua mkutano mkuu wa wakuu wa majeshi ya polisi, Afrika mashariki

Leo jumatano, Rais Paul Kagame amefungua mkutano mkuu wa wakuu wa majeshi ya polisi katika mataifa ya Afrika mashariki EAPCCO (Eastern African Police Chiefs Cooperation Organization) unaolenga kujadili maswala ya udukuzi na kutafuta namna ya kukomesha uhalifu huo.

Akifungua huu mkutano, Kagame amesema kuwa kushirikiana na Interpol kunahitajika ili kujikingia uhalifu amabao huvuka mipaka na alionya washiriki kuwa hata hata ingawa wakuu wamajeshi ya polisi hawatakutekeleza vyema utaratibu wa kupambana na wadukuzi, maendeleo Afrika yalioyapata huenda akatetereka.

Rais Paul Kagame aliongeza kuwa teknolojia ya kisasa ndio silaha halisi kwa mapolisi inayoweza kutokomeza uhalifu hufanyika kwenye intaneti.

Huu mkutano ambao umefunguliwa leo mjini Kigali na unatarajia kumalizika tarehe mbili mwezi ujao.

Nchi wanachama wa EAPCCO ni Rwanda (nchi mwenyeji wa mkutano), Burundi, Sudan, Sudan kusini, Ethiopia, Uganda, Eritrea, Seychelles, Comoros, Somalia, Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Kenya na Djibouti.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments