CHADEMA wasitisha maandamano ya UKUTA

Freeman
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesitisha maandamano ya UKUTA ambayo yalipangwa kufanyika Septemba 1 (kesho) baada ya kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa viongozi wa dini.

Akiongea na waandishi wa habari muda huu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema chama kimeona kisitishe maandamano kwa muda ili kiwaachie viongozi wa dini watafute suluhu kuhusu suala hilo.

“CHADEMA tunaomba kuwatangazia watu wote kwamba tunahairisha mikutano ya kisiasa na maandamano yote kwa muda wa mwezi mmoja,” alisema Freeman Mbowe

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments