Wanawake wakulima kufadhiliwa $ 12 milioni kwa kuimarisha ongezeko la mazao

Edna Kalima kutoka NEPAD na Mutono Gatsinzi wa MIGEPROF
Wizara ya mipango ya familia na usawa wa jinsia inasema kwamba aendako kupa wanawake wakulima wadogo $ 12 milioni zilizotolewa na NEPAD kwa ajili ya kuwasaidia kupambana na mabadiliko ya anga.

Huu msaada ulitangazwa katika mazungumzo kati ya MIGEPROF na NEPAD kupitia tawi la GCCASP (the gender climate change Agriculture support program) jana jumanne, mwezi huu.

Akifungua mazungumzo, Katibu wa serikali katika MIGEPROF, Mutoni Gatsinzi Nadine amefunguka kuwa idadi ya wanawake ni asilimia 52 ya wanyarwanda na kuwa zaidi ya asilimia ya 80 ya wanyarwanda ni wakulima, hii inamaanisha kuwa wanawake wakulima wadodo hawawezi kusahaulika.

Dola hizi zinatarajiwa kutumiwa kwa kuwanunulia vifaa vya umwagiliaji, mbolea na mbegu.

Kwenye ajenda yake, NEPAD alichagua kupa nguvu za kilimo mataifa yakiwemo Rwanda, Naijeria, Cameroon, Etrhiopia na Malawi kutokana na hamu ya kila nchi kwa kumpa uwezo mwanamke.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments