Mchezaji wa AZAM Fc yaunga mkono pendekezo la kuajiri mnyarwanda kama kocha mkuu wa timu ya taifa

Mugiraneza Jean Baptiste ajulikanae Migi ambaye ni mchezaji machachari wa timu ya taifa Amavubi na pia mchezaji wa timu ya AZAM ( Tanzania) anatangaza kuwa huu ni muda wa kupa nafasi kocha mzalendo ili aoneshe wanyarwanda uwezo wake kwani makocha wa ugenini hawajaleta mambo mapya.

Kwa sasa timu ya taifa inaongozwa na Jimmy Mulisa na kocha wake msaidizi ni Mashami Vincent na Higiro Toma ambaye ni mkuzunzi wa walinda goli.

”Huu ndio muda sahihi, miaka kadhaa inapita tukiwa na makocha kutoka ugenini lakini tumeona kuwa hakuna kitu zaidi walichofanya kuliko makocha wa ndani. mimi natumai kuwa hiii ni nafasi nzuri ya makocha wanyarwanda ili watuonyeshe yale walioyasoma”. Mugiraneza alisema.

Isipokuwa mchezaji huyo alisema haya kama maoni yake, waziri wa Utamaduni na michezo Uwacu Julliene ametangaza kuwa hakuna kocha mzalendo mwenye uwezo wa kusimamia timu ya taifa kama kocha mkuu lakini aliongeza kwamba wataendelea kuwatetea na kuwapa masomo yatakayowapandisha ngazi.

Wakati makocha Mulisa na Mashami walipopewa majukumu haya, wizara ya Michezo na utamaduni (MINISPOC ) ilitangaza kuwa wataifunza timu hii katika mechi dhidi ya Ghana tu na watamtafuta kocha mkuu baadaye.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments