Rais Kagame aonyesha ndoto za kuimarisha utalii barani Africa

Katika mazungumzo na Rais Patrice Talon wa Benin katika, Paul Kagame amesema kwamba yeye ana ndoto za kuhimiza waafrika kutembelea nchi za Afrika kama walitembelea mataifa mengi Duniani kote yasio ya Afrika.

‘’waafrika walizunguka dunia kote ukiondoa nchi za Afrika, ndoto zangu ni kuumba uhusiano wa utalii na kubadilishana.’’ Kagame amesema.
Patrice Talon amesama kuwa Rwanda ni nchi ni iliyonesha kuwa wakati wowote una nia, unapata ushindi.

‘’nchi hii imenionyesha kwamba wakati una nia na dhamira unaweza kushinda kuliko wengine.’’ Talon amesema.

‘’sisi hatuko watu waliolaaniwa, Rwanda ilionyesha mfaano.’’ Talon ameongeza.

Rais Patrice Talon wa Benin yuko ziarani ya siku tatu nchini Rwanda baada ya kufika jana jumatatu.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments