‘’Alama ya viapo si kama alama ya darasani.’’ Meya wa wilaya iliyoshika mkia mwaka jana

Nzamwita Deogratias ambaye ni meya wa wilaya ya Gakenke, Kasikazini mwa Rwanda anasema kuwa ana matumaini ya kuwa wilaya haitakuwa ya mwisho kamwe kwenye orodha ya wilaya zilizofanya vibora, na aliongeza kwamba alama ya viapo vya wilaya si akama yale alama ya darasani.

Meya Deogratius anasema hayo baada ya wilaya yake( Gakenke ) kushika nafasi ya mwisho 2014/15 na 2010/2011 kwenye oradha ya wilaya zilizotekeleza vibora mipango yao kwa ajili ya kuimarisha maisha ya raia wa chini.

Mwanzoni mwa mwezi Agosti, mameya wa wilaya zote (30) wanatarajiwa kusaini mapatano ya mwaka wa 2016/2017 na Rais Paul Kagame na kumuonesha namna walivyotimiza ndoto zao za mwaka jana.

Akiongea na Makuruki.rw, Deogratius amesema kwamba nafasi wilaya yake iliyoshika mwaka uliopita si ya kujivunia na wao wanataka hivyo kutokuwa tena.

‘’alama ya viapo si kama alama ya darasa, kila wilaya inabeba mzigo wake, je, wewe unaweza kusema acha mimi niwe wa nyuma ? Ni kosa kulinganisha wilaya iliyokumbwa na mafuriko na wilaya nyingine lakini nasi tuantaka kuwa wa kwanza.’’

Akionyesha matumani ya kutoshika mkia tena, Meya Nzamwita anasema kwamba wao wanalenga kukuza miundombinu.

Ingawa ya wilaya ya Gakenke kuwa ya mwisho mara mbili, ilikuwa nafasi ya nne katika mwaka wa 2012/2013.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments