UNDP yatahadharisha kuhusu usawa wa kijinsia Afrika

Umoja wa Mataifa umezitolea wito nchi za Kiafrika kufanya jitihada za kujaza pengo la usawa wa kijinsia katika nchi hizo pengo ambalo kila mwaka husababisha hasara ya dola bilioni 95 kwa nguvu za kiuchumi.

Hellen Clark Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) alisema jana Jumapili kuwa jamii zinabaki nyuma kimaendeleo katika maeneo ambayo kunakuweko pengo kubwa la usawa wa kijinsia. Bi Hellen ameongeza kuwa jamii hizo hazinufaiki na uwezo kamili wa wanawake na kwamba suala hilo husababisha madhara makubwa kwa uchumi katika ngazi ya familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango Maendeleo (UNDP) ameashiria kilimo kuwa moja ya mfano wa kazi ambayo wanawake katika nchi nyingi za Kiafrika wanashindwa kumiliki au kurithi na kubainisha kuwa, jambo hilo huwafanya wanawake kushindwa kupata mikopo kwa urahisi.

Shirika la UNDP limeeleza kuwa, kukosekana usawa wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume katika nchi za Kiafrika chini ya jangwa la Sahara kila mwaka husababisha hasara ya dola milioni 95 kwa sekta ya uchumi ya bara hilo.

UNDP imeongeza kuwa mwaka 2014 kiwango cha hasara iliyosababishwa kwa sekta ya uchumi kilikuwa cha juu na kufikia dola bilioni 105. Bi Hellen Clark ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani wa New Zealand na mgombea wa kiti cha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameashiria pia maendeleo katika baadhi ya nchi za Kiafrika kama Rwanda na kueleza kuwa asilimia 65 ya wabunge wa nchi hiyo ni wanawake.

Chanzo:ParsToday

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments