Rwanda kutumia Rwf 5.5 bilioni kwa ajili ya uchaguzi urais mwaka ujao

Tume ya uchaguzi inasema kuwa Serikali ya Rwanda itatumia Rwf 5.5 bilioni kwa kufadhili uchaguzi urais unaopangwa kufanyika mwezi Agosti,2017.

NEC (National Electral Commission) inasema kwamba kiasi cha bajeti kupunguzwa ukilinganisha na karibu na Rwf 7 bilioni zilizotumika katika uchaguzi urais wa mwaka 2010.

Katibu mtendaji wa NEC alisema kwamba wao watatumia vifaa vya uchaguzi vilivyotumiwa miaka ya nyuma na kuanzishwa kwa teknolojia katika uchaguzi. Na aliongeza kuwa bajeti ya mwaka ujao itakuwa maradufu ya bajeti ya mwaka wa 2003.

Akiongea na gazeti la The newtimes, Charles Munyaneza alisema kuwa uchaguzi unatarajiwa kutimua vumbi mwezi Agosti wa mwaka wa 2017 kama katiba ya Rwanda inavyosema lakini NEC hakuwekwa tarehe ya uchaguzi hadhara.

Kwa mujibu wa NEC, idadi ya wapiga kura ni milioni 6.6, ongezeko la 1.4 kutoka mwaka 2010 na milioni 3.9 za walioshiriki uchaguzi wa mwaka 2003.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments